ISBN 9789987449866
Pages 262
Dimensions 198 x 129mm
Published 2022
Publisher Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Format Paperback

Peponi

by Abdulrazak Gurnah, Dr. Ida Hadjivayanis

Swahili translation of the Nobel-prize winning author's 1994 novel Paradise.

Mzaliwa wa Afrika ya Mashariki, Yusuf anaondoka kwao kwa ghafla akiwa na umri wa miaka kumi na mbili. Haimjii hata kwa sekunde moja, kwamba atakuwa mbali na wazazi wake kwa muda mrefu, na wala hafikirii kuuliza atarudi lini au kwa nini safari iliandaliwa kwa ghafla kiasi kile. Yusuf anaamini kuwa anamsindikiza Ami Aziz lakini ukweli ni kwamba ‘ami’ yake ni Mfanyabiashara, tena tajiri mkubwa, na Yusuf amewekwa rehani ili kulipia madeni ya baba yake.

Yusuf anajikuta anasafiri katika miji na vitongoji vingi vingine ambako anakutana na watu wa kila namna. Anabalehe na kukua kwenye dunia inayobadilika kwa kasi kutokana na kuingia kwa ukoloni na udhalimu wake na jamii kuharibika kwa kuvurugwa kwa utamaduni wake.

Hii ni tafsiri ya kwanza kwa riwaya za Abdulrazak Gurnah katika lugha ya Kiafrika.

Abdulrazak Gurnah ni mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya mwaka 2021. Ameandika riwaya kumi ikiwemo hii ya paradise. Gurnah ni Profesa wa Masomo ya Kiingereza na Fasihi za Kikoloni katika Chuo Kikuu cha Kent.

Dkt. Ida Hadjivayanis ni Mhadhiri Mwandamizi wa Masomo ya Kiswahili SOAS, Chuo kikuu cha London. Ametafsiri riwaya kadhaa kwa Kiswahili na Kiingereza.
Book Preview
Paperback
£18.70
eBook
£18.70

About the Author

Abdulrazak Gurnah

Abdulrazak Gurnah was awarded the Nobel Prize in Literature in 2021. This is a Swahili translation of his 1994 novel, Paradise. The translator is Ida Hadjivayanis, Senior Lecturer in Swahili Studies, SOAS University of London.