ISBN | 9781068620591 |
Pages | 76 |
Dimensions | 279x216 mm |
Published | 2024 |
Publisher | AdelPhil Consultancy, Tanzania |
Format | Paperback |
Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
by Evarist Chahali
In the compelling nonfiction book, "Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?", a former intelligence officer takes you on an eye-opening journey into the clandestine world of intelligence operations. Delving deep into the profession, from its core definitions to the rigorous recruitment processes and intense training regimes of intelligence officers, this book offers a comprehensive look at what it truly means to be a guardian of national security. Through the lens of both Tanzanian and global contexts, readers will uncover the intricate details of a day in the life of an intelligence officer, along with the formidable challenges faced in this high-stakes profession. A must-read for intelligence professionals and an enlightening resource for non-intelligence readers seeking a deeper understanding of the covert realms that shape our world.
Ukosefu wa machapisho kuhusu taaluma ya uafisa usalama wa taifa umechangia sana mkanganyiko katika jami kuhusu ushushushu na mashushushu huku baadhi wakiamini kwa dhati kabisa kuwa taaluma hiyo inahusika na 'mambo mabaya tu,' kama vile kuuwa watu wasio na hatia, umumiani (kunyonya damu kama 'vampires') na hisia potofu kama hizo.
Kwahiyo kitabu hiki, bila kukiuka kanuni na sheria za usiri zinazotawala taaluma hiyo, kinajaribu kufungua ukurasa mpya, angalau kwa huko nyumbani, kutoa picha ya jumla kuhusu taaluma hiyo muhimu mno kwa usalama na ustawi wa taifa letu, sambamba na kuelezca kwa undani mchango muhimu wa mashushushu kwa usalama wa taifa letu, ikiwa ni pamoja na kubainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili, na kutoa mapendekezo ya kuzikabili.
Kwa 'nchi za wenzetu, mashushushu wa zamani au wastaafu wamekuwa vyanzo vikuu vya uelewa kuhusu fani hiyo nyeti ambapo wamekuwa wakiandika vitabu mbalimbali, ihali wengine wakishirikiana na sekta ya filamu katika utengenezaji wa filamu zinazohusu ushushushu. Kwa bahati mbaya (au pengine kwa makusudi tu), kwetu ile kuzungumzia tu jambo lolote linalohusu ushushushu ni kama mwiko au dhambi. Kasumba hiyo imeawaathiri hata wanataaluma ambao hawajawahi kujihusisha kufanya tafiti au kuandika machapisho ya kitaaluma kuhusu fani hiyo.
Uhaba wa 'references' unatoa kisingizio kizuri kwa wasomi wetu 'kupuuzia' mada hiyo muhimu. Kimsingi, taaluma ya ushushushu inatawaliwa na usiri, na mengi ya yanayohusiana na taaluma hayo yanabaki kuwa siri. Hata hivyo, kuna maciezo ambayo yapo wazi japo inahitaji uelewa wa aina flani kuchora mstari kati ya kipi ni siri na kipi ni ruksa kuwa hadharani.