ISBN 9789987753840
Pages 196
Dimensions 198 x 129 mm
Published 2022
Publisher Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Format Paperback

Bweni la Wasichana

by Lucas Lubango

Usiku huo nilikuwa nasimamia maandalizi ya masomo ya usiku. Nikapigiwa simu na Rose, nikaipokea. Wakati naongea naye, nikawa natembea taratibu kama naelekea kwenye mabweni. Ghafla, nikaona taa za bweni wanalolala "Buibui" zinawaka na kuzima, nikajua ni hitilafu katika mfumo wa umeme. Nikataka kusogea ili nithibitishe kisha nitoe taarifa mapema kwa uongozi na matengenezo yafanyike. Nilisogea mpaka mlangoni, taa zikawaka moja kwa moja, na kwa kuwa kulikuwa na dalili za kuwemo mwanafunzi, nilitaka kujua kwanini hayupo darasani wakati wenzake wote walikuwa wana-jisomea. Nilingia nikakuta hali ya ukimya sana, nikatembea mpaka karibu na mwisho wa bweni, nilichokiona ni aibu kubwa! Huwezi amini, "Buibui" waliponiona wakadondosha khanga! Wakabaki kama walivyozaliwa..

Book Preview
Paperback
£19.80