ISBN 9789987753659
Pages 76
Dimensions 198 x 129 mm
Published 2022
Publisher Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Format Paperback

Chemchemi Jangwani

by Mohamed Omar Juma

Jangwa lenye jua kali, Navyo vivuli vichache, Vya miti isiyo hali, Jua linatoa cheche, Safari yenye machofu, Pepo kurusha mavumbi, Wengine wamepofuka. Tumshukuru jalali, Ameiotesha miche, ya miti yenye vivuli, Vya wengi sio wachache, Kiu ilipo- tukifu, Hapo ikabubujika, Chemchemi jangwani. Ni chemchemi jangwani, Yenye maji ya kutosha, Mwenye kiu kukatisha, Mwenye uchafu akoge, Ama ajitoharishe, Majumba yapigwe deki, Nafsi zisuuzike. Maji yaliyosafika, Yenye asili rutuba, Twapata matumaini, Miti yote itashiba, Bustani kupendeza, Na mifugo kunawiri, Videge kuchezacheza, Wala haizuiliki, Mola aipe kibali, Jangwani itamalaki, Walimwengu iwafae, Wagonjwa iwatibie, Joto nalo lififishwe, Kwa Chemchemi jangwani.

Book Preview
Paperback
£16.50