ISBN 9789987084975
Pages 184
Dimensions 198 x 129 mm
Published 2022
Publisher Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Format Paperback

Kilio cha Mwanamke

by Idrissa Haji Abdalla

Sauti dhaifu ya kilio cha mwanamke ilinifikia pale nilipokuwa nimesimama karibu na vichaka vikubwa vilivyoshonana mbele yangu. "Hivi ni sauti ya binadamu kweli au ni mlio wa mnyama fulani?" Nilijiuliza swali hilo ingawa sauti ile niliyoisikia ilifanana sana na kilio cha mwanamke ambaye yuko katika maumivu makali. Hali fulani ya woga ilianza kuniingia polepole. Baada ya kuanza kupatwa na woga niliamua kumfuata bibi yangu ambaye nilimwacha akiendelea kukata kuni nyuma ya vichaka vingine vilivyokuwa kushoto kwangu. Baada ya kutembea kwa hatua zisizozidi kumi nilimwona bibi akinifuata. Hapo niliamua kusimamana kumsubiri ili nim-wulize juu ya ile sauti niliyoisikia. "Nimesikia sauti kama ya mtu ambaye alilia kwa muda mrefu na mwisho akapoteza nguvu". Bibi yangu alieleza hivyo kabla ya mimi kumweleza. "Hata mimi nilisikia ile sauti, tena inaelekea ni sauti ya mwanamke. Hivi unavyoniona ndio nimeamua kutofuata tena hizo kuni, maana nimeanza kuogopa.”

Book Preview
Paperback
£19.80