ISBN | 9789987083183 |
Pages | 234 |
Dimensions | 198 x 129mm |
Published | 2018 |
Publisher | Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania |
Format | Paperback |
Kikosi cha Kisasi
by E.A. Musiba
Mauaji ya kikatili yanafanyika karibu na mji wa Uitenhage nchini Afrika Kusini siku ya kuwakumbuka wazalendo, waliouawa mjini Sharpeville mwaka 1960. Makaburu wanajawa na hofu kwa mauaji hayo, na wanawatilia shaka kikundi cha watu weusi wanaotaka kupindua mfumo wa Serikali yao ya Ubaguzi wa Rangi. Uongozi wa Makaburu wa Afrika Kusini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika la Ujajusi, Kamanda wa Jeshi la Kulfut na Mkuu wa Magaidi, na wasaliti wa UNITA, wanakutana ili kukabili juhudi za ukombozi wa Afrika Kusini kwa wimbi la mauaji. Mkutano wa Wapigania Uhuru wa Afrika Kusini unafanyika Arusha, nchini Tanzania. Mpelelezi nguli wa Afrika, Willy Gamba, hakosi panapokuwa na mapambano kati ya upande wenye haki, upande wa umma na ule wa dhuluma. Kwa kushirikiana na wapelelezi mahiri kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kwa kutumia medani za kivita, mateke, ngumi, kung fu achilia mbali bastola, visu na silaha nyingine wanapambana dhidi ya Makaburu hao na vikundi mbalimbali vya kigaidi vilivyoshirikiana nao.