ISBN 9789987753703
Pages 132
Dimensions 198 x 129 mm
Published 2022
Publisher Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Format Paperback

N’na Kwetu

Sauti ya Mgeni Ugenini

by Mohammed Khelef Ghassani

Tungo nyingi zilizomo humu ziliandikwa baina ya robo ya mwisho ya mwaka 2010 na nusu ya mwanzo ya mwaka 2015. Hii ni miaka mitano ya mwanzo ya mshairi kuhamia na kuishi nchini Ujerumani - mbali na nyumbani kwao, Zanzibar. Ndani yake, kwa hivyo, muna muakisiko wa hisia za mgeni ugenini, akitayamani mengi mazuri ya kwao na akijutia kuyaacha nyuma yake. Ukweli ni kuwa wakati mtu anapoishi ugenini, ndipo hasa ile thamani ya kwao anapoitambua na kutaka kuitambulisha navo zaidi na zaidi. Ndipo hisia za kutambuwa kuwa ana kwao zinapopanda kiwango cha juu. Kutoka kipembe cha mbali, Mohammed Ghassanani anakuangalia kwao na kuyaona mambo ambayo alipokuwamo ndani yake, alikuwa hata hajui kama yapo. Chembilecho Wajapani: "Samaki hajijui kuwa amerowa!" Na sababu ya kutokujijuwa huko, kwa hakika, ni kwa kuwa yeye mwenyewe anaishi ndani ya maji muda wote.

 

Book Preview
Paperback
£19.80

About the Author

Mohammed Khelef Ghassani

Mohammed Khelef Ghassani alizaliwa mwaka 1977 visiwani Zanzibar na ni mwandishi wa diwani kadhaa za ushairi, zikiwemo Andamo: Msafiri Safarini, Siwachi Kusema: Uhuru U Kifungoni, Kalamu ya Mapinduzi: Mapambano Yanaendelea na N'na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini, ambayo ndiyo iliyompatia tuzo ya Fasihi ya Kiafrika kwa Lugha ya Kiswahili iliyotolewa na Mabati-Cornell mwaka 2015. Mbali na kuwa mshairi, Mohammed Ghassani ni mwandishi wa habari anayeishi na kufanya kazi zake nchini Ujerumani.