ISBN 9789976973914
Pages 132
Dimensions 230mm x 147mm
Published 2002
Publisher Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Format Paperback

Maisha ya Mchagga hapa Duniani na Ahera

by Petro Itosi Marealle

Mangi Petro Itosi Marealle, aliyekuwa Mangi Mwitori wa Vunjo, amewafanyia kabila la Wachagga na wazao wa baadaye, kazi ya maana sana kwa kuandika kitabu hiki juu ya desturi za Wachagga kabla hazijatoweka na kupotea. Alijitolea miaka mingi kujifunza kwa uangalifu mila na desturi hizi, na alipata mashaka katika kutafuta njia ya kukichapa kitabu hiki. Ninafurahi kusema amekwisha pata njia. Natumaini kitabu hiki hakitapendwa na Mchagga tu, lakini kila mmoja atakaye kujifunza maendeleo ya Wana-Adamu, na natumaini kitaamsha Wa-Africa wa makabila mengine kutunga habari za namna hii za watu wao. Mwandishi wa kitabu hiki Marehemu Mangi Petro Itosi Marealle alikuwa Mangi wa Marangu kuanzia mwaka 1931 hadi 1946, na ‘Mangi Mwitori’ wa Vunjo hadi mwaka 1961. Umangi ulipofutwa mwaka 1962 alishika wadhifa mbalimbali katika Halmashauri ya Wachagga na wadhifa wake wa mwisho ulikuwa kama Mwentekiti wa Tume ya Serikali za Mitaa. Aliafriki mweai Mei, 1982.

First published in 1947, this is a comprehensive explanation of the customs and traditions of the Chagga people by the Paramount chief of the Chagga people of Kilimanjaro, Tanzania. 

Book Preview
Paperback
£26.00

Related Books