ISBN 9789987753932
Pages 254
Dimensions 198 x 129mm
Published 2017
Publisher Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Format Paperback

Mungu Hakopeshwi

by Zainab Alwi Baharoon

Riwaya ya Mungu Hakopeshwi inaelezea maisha ya familia moja ya Unguja iliyoingia katika mitafaruku na mikasa mingi. Kila kitu huwa na chanzo na khatima; basi ni nini chanzo cha mitafaruku hiyo na khatima yake ilikuwaje? Simulizi ni juu ya baba, Bw. Ahmed, mwenye hasira kali zisizo na mipaka, aliyeongoza familia yake kwa utashi wa nafsi yake, bila kujali hisia za mkewe wala wanawe. Kumbe moyoni mwake alihifadhi siri, na hiyo siri ndiyo iliyomfanya Bw. Ahmed kuwa mkali bila kiasi, ikimsukuma azuie kurejea kwa yale yaliyomfika zamani. Lakini kivuli cha historia ya maisha yake ya nyuma hakikuacha kumuandama. Riwaya hii i meandikwa kwa lugha nzuri na fasaha, kwa ufundi wa msanii makini na mwelewa wa maisha ya jamii za Kizanzibari na za mwambao kwa jumla.

Book Preview
Paperback
£18.20
eBook
£17.33

Review

“In Mungu Hakopeshwi, Zainab Alwi Baharoon, has used the standard unguja Swahili masterfully. The language used flows so effortlessly that the  reader can also have fun while reading. The overriding issue handled in this work is women’s struggles against the backdrop of male chauvinism and domination where the women find themselves at the bottom rung of the societal ladder (especially in the Swahili society).”

Mabati Cornell Kiswahili Prize

About the Author

Zainab Alwi Baharoon

ZAINAB ALWI BAHAROON alizaliwa Mji Mkongwe, Zanzibar. Licha ya umri wake anaonesha katika riwaya hii dalili zote za kipaji cha uandishi wa riwaya, na kuwa kazi zake zitakuja kushamiri na kumpandisha kwenye jukwaa la waandishi maarufu.Hii ni riwaya yake ya mwanzo.