ISBN 9789987084869
Pages 236
Dimensions 303 x 220
Illustrations Colour Illustrations and Colour Photographs
Published 2021
Publisher Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Format Hardback

Vipande vya Dinosaria

Historia ya Msafara wa Kpaleontolojia Kwenda Tendaguru Tanzania 1906 – 2018

by Ina Heumann, Holger Stoecker, Mareike Vennen

Kitabu hiki kinasimulia habari za msafara wa kisayansi na nyara zili-zopatikana kwenye msafara huo. Masimulizi haya yanaanzia mwan-zoni mwa karne ya ishirini, katika kilima cha Tendaguru, kusini mwa nchi ambayo sasa inaitwa Tanzania lakini wakati huo ilikuwa koloni la Wajerumani lililojulikana kama Deutsch-Ostafrika. Mnamo mwaka 1907, habari za uvumbuzi wa kusisimua wa mifupa, katika kilima cha Tendaguru, ziliufikia Ufalme wa Ujerumani. Muda mfupi baa-daye, ikafahamika kwamba kilichovumbuliwa ni visukuku vya mifupa ya dinosaria wakubwa ajabu, wenye ukubwa ambao haujawahi kuo-nekana, ambao waliishi duniani miaka milioni 150 iliyopita na walik-wisha kutoweka. Miaka  michache baadaye, msafara ulioongozwa na wanasayansi wa Kijerumani, ulikwenda  mahali hapo na kufanikiwa kuchimbua tani 250 za visukuku vya mifupa hiyo ya wanyama wa zama za kale. Mojawapo ya mapato ya uchimbuaji huo ni kiunzi maa-rufu kiitwacho Graffatitan brancai ambacho kimewekwa kwenye mao-nesho ya Jumba la Makumbusho ya Historia ya Asili, Berlin. Kitabu hiki kinafuatilia  hatua kwa hatua mwendo wa visukuku hivyo kutoka kilima cha Tendaguru kwenda pote vilikofikishwa, katika kipindi cha karne ya ishirini. Sura za kitabu hiki, kwa kutegemea vyanzo vya ha-bari kutoka hifadhi za  nyaraka za Tanzania, Ujer umani na Uingereza, pamoja na mahojiano, zinauliza, ni kwa jinsi gani historia ya msafara huo imekuwa ikisawiriwa hadi wakati wa sasa. Kitabu kinaonesha jinsi historia ya nyara hizo zilizopatikana Tendaguru inavodhihirisha muingiliano baina ya siasa, sayansi na majumba ya makumbusho, ulivyoyapa sura majadiliano na mabishano; mawasilisho na ufahamu uliopo hadi leo kuhusu Giraffatitan brancai.

Book Preview
Hardback
£30.00

About the Authors

Ina Heumann

Ina Heumann aliongoza mradi wa “Dinosaria huko Berlin”. Anafanya kazi kama mwanahistoria wa sayansi na mweledi wa Historia ya Kipindi Tulichonacho sasa, katika Jumba la Makumbusho ya Historia ya Asili, Berlin. Utafiti wake umejikita katika Siasa ya Historia ya Asili Katika Karne ya Ishirini.

Holger Stoecker

Holger Stoecker ni mwanahistoria na alifanya uchunguzi akiwa Idara ya Masomo ya Kiafrika ya Chuo kikuu cha Humboldt, Berlin, kuhusu historia ya wakati wa ukoloni inayoohusu dinosaria wa Afrika walioko Berlin. Vilevile anashughulika na uchunguzi kuhusu historia ya ukoloni na sayansi kati ya Afrika na Ujerumani na pia utafiti kuhusu asili ya nyara zilizokusanywa kutoka Afrika wakati wa ukoloni.

Mareike Vennen

Mareike Vennen alifanya kazi kwenye mradi huu kama mshiriki kutoka katika Taasisi ya Masomo ya Sanaa na Masomo ya Historia ya Miji, ya Chuo Kikuu cha Ufundi cha Berlin. Yeye ni mwanasayansi wa tamaduni na anatafiti historia ya ufahamu na nyenzo za habari na mawasiliano katika historia ya asili na vile vile anatafiti kuhusu ukusanyaji wa nyara na tamaduni za makumbusho wakati wa karne ya kumi na tisa na ishirini.