ISBN 9789987084081
Pages 162
Dimensions 198 x 129mm
Published 2020
Publisher Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Format Paperback

Vitimbi vya Mama wa Kambo

na hadithi nyingine

by Ally Yusufu Mugenzi

Vitimbi vya Mama wa Kambo, Wivu, Radhi za Wazazi, Ra ki Maluuni, Mchumba Kaka na Adui Mama ni hadithi zinazosawiri jamii alimochipukia mwandishi, au kuishi na kufanya kazi akiwa polisi, mwandishi wa habari na mtangazaji wa redio katika nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi na Uingereza kwa takriban miaka 40. Kitabu hiki ni matokeo ya maombi ya watu wengi waliomsikiliza akizisimulia katika kipindi cha Hadithi na Muziki cha Redio Rwanda katika miaka ya 1980 na 1990. Hadithi hizi pia zimekuwa zikitumiwa na wakuza mitaala wa Kiswahili nchini Rwanda shuleni na zimewafurahisha wapenzi wengine wa fasihi nje ya shule.

Book Preview
Paperback
£17.60

About the Author

Ally Yusufu Mugenzi

Ally Yusufu Mugenzi kwa jina jingine Ally Kayamba alijiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari Tanzania mwaka 1978. Alipohitimu mwaka 1980, aliajiriwa na Shirika la Habari Tanzania - SHIHATA.  Mwaka 1983 aliacha kazi SHIHATA akajiunga  na  Idhaa ya Kiswahili ya Redio Rwanda.  Mwanzoni mwa mwaka 1994, aliacha  kazi Radio Rwanda  alipoajiriwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC-London. Akiwa BBC, alianzisha idhaa ya kukutanisha watu waliotenganishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda. Baadaye ilibadilika na kuwa Idhaa ya Maziwa Makuu. Mwaka 2005 aliteuliwa kuwa mhariri wa idhaa hiyo  ambako yuko mpaka sasa.