ISBN 9789987083268
Pages 192
Dimensions 203 x 133mm
Published 2017
Publisher Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Format Paperback

Diwani ya Tuzo ya Ushairi ya Ebrahim Hussein

by Juzuu la Pili

Diwani hii ni matunda ya shindano la pili la Tunzo ya Ushairi ya Ebrahim Hussein lililofanyika mwaka 2015/16. Tunzo hiyo ilianzish- wa na hayati Gerald Belkin, muongoza filamu aliyekuja Tanzania kutengeneza filamu juu ya maisha na changamoto za ujenzi wa ujamaa vijijini miaka ya 1960 na 1970. Belkin alifanya kazi bega kwa bega na Profesa Ebrahim Hussein, mwanazuoni maarufu na mwandishi wa tamthilia na  mashairi. Kupitia kwa Hussein, Belkin alivutiwa na utamaduni wa Kiswahili, hususani ushairi. Katika wosia wake, kabla ya kufikwa na mauti, aliacha fungu la fedha ili zitumiwe kushindanisha washairi wa Tanzania, na tunzo itolewe kwa washindi watatu wa kwanza.  Belkin alianzisha tunzo hii ili kuuenzi mchango wa rafiki yake, Ebrahim Hussein, katika kuijenga fasihi ya Kiswahili.

Ebrahim Hussein ametoa mchango mkubwa katika utunzi, uchambuzi na falsafa ya fasihi. Vitabu vyake, kwa mfano Kinjeketile , Mashetani , Wakati Ukuta na Kwenye Ukingo wa Thim vimebeba fikra nzito juu ya migogoro ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni inayotokana na mabadiliko ya kihistoria nchini Tanzania na barani Afrika kabla na baada ya uhuru. Ni jambo la kusikitisha kuwa kazi hizo bora hivi leo hazipatikani kwa wingi wala kufundishwa shuleni nchini Tanzania.

Diwani hii ni chapisho la pili la Tunzo ya Ebrahim Hussein. Bodi ya Tunzo iliamua kwamba tungo bora za shindano kwa kila awamu ziwe zikichapishwa katika Diwani ili ziweze kusomwa na watu wengi zaidi. Hivyo, Diwani hii maalumu ya pili ina mashairi teule ya washin- di na washiriki wengine wa shindano, pamoja na tafsiri za Kiingereza za mashairi ya washindi watatu wa kwanza. Diwani nyingine zitaku- wa zikichapishwa kadiri shindano linavyoendelea kufanyika.

Mashairi haya yametungwa na washairi mchanganyiko – vijana, watu wazima, wazee, wanawake, wanaume, wafanyakazi, wasomi, wakulima, n.k. Kwa pamoja, mashairi haya yanatusawiria hali ya Tanzania na Afrika katika kipindi hiki, na kubainisha mitazamo anuai ya wananchi wa kawaida kuhusu hali hiyo na kuhusu mustakabali wa nchi yao na bara lao la Afrika. Diwani hii inafaa kusomwa na watu wote wanaojali hali na hatima ya Mwafrika.

This is the second collection of poems that were entered for the Ebrahim Hussein poetry prize for 2015/2016. The late Gerald Belkin, film director, who came to in order to record on film the challenges of building Ujamaa (socialist) villages in the sixties and seventies established the prize fund.

Book Preview
Paperback
£23.10

Related Books